Na hii ndio aina ya kiongozi ambae watanzania wanamtarajia leo. Kiongozi hodari na shupavu katika uadilifu na utendaji kazi ambae ana uwezo wa kukimbizana na kasi ya maendendeleo inayoendana na dunia ya leo. Katika mbio hizi za uchaguzi mkuu, kiongozi huyo sio mwingine bali ni Dr. John Pombe Magufuli.
Mapema wiki hii akiwa mkoani Tabora pamoja na mengi, alitoa ahadi zifuatazo kwa wananchi wa Tanzania mara atakapo chaguliwa kuwa Rais wao.
Alisema," Watarajie utumishi uliotukuka, watarajie uongozi wa hali ya juu, watarajie uchapa kazi. Watarajie serikali itakayokuwa ina amua haraka na kutenda haraka. Lakini sio tu uamuzi wa haraka na utendaji wa haraka bali pia uamuzi sahihi na utendaji sahihi. Watarajie serikali imara itakayosimamia maslahi ya umma. Watarajie uongozi wa kidemokrasia lakini pia watarajie uwepo wa nidhamu kwenye serikali na jamii nzima.
Watarajie kwamba nitasimamia utawala wa sheria , kwamba hakuna mtu atakaye kuwa juu ya sheria na hakutakuwa na mzaha wala majadiliano katika kufuata sheria za nchi. Wasitarajie sherehe wala hafla nyingi kutoka kwangu.
Wasitarajie propaganda za ujanja ujanja kutoka katika serikali yangu bali ukweli wakati wote. Watarajie kwamba nitakuwa nikifuatilia mambo mengi kwa kina, mimi mwenyewe.
Watarajie kwamba nitalinda umoja, amani na usalama wa nchi yetu kwa nguvu zote. Watarajie kwamba nitakuwa kiongozi wa wote bila kubagua mkoa, kanda, dini, kabila wala vyama."
Katika kinyang'anyiro cha urais wanaotarajia Watanzania October 25, hakuna kiongozi mwingine ambae ana uwezo wa kufanya vizuri na mwenye sifa za utekelezaji wa uhakika kama Dr. Magufuli. Ahadi zake ni za kweli, makini, na zinatekelezeka. Ama kwa hakika historia inajieleza, ANAWEZA.
Chagua Magufuli, " HAPA KAZI TU!".
M4C(MAGUFULI 4 CHANGE)
Latest
Previous
Next Post »
Next Post »
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
EmoticonEmoticon