Imedhihirika kwamba mgombea wa urais kwa tiketi ya UKAWA kupitia CHADEMA, ndugu Edward Ngoyai Lowassa hawezi kujibu maswali na hoja mbalimbali zinazo ulizwa na wananchi katika kampeni zinazoendelea hivi sasa. Mgombea huyo ameonekana akikwepa maswali mbali mbali na tuhuma ambazo zimekuwa zikielekezwa dhidi yake. Badala ya kujibu amekuwa akichagua kipi ajibu na kipi asijibu hata kama ni mambo ya msingi yanayo hitaji majibu na ufafanuzi wa dhati kwa wananchi.
Mathalani hivi majuzi alipokuwa katika kampeni zake mkoani Dodoma pale Mvumi jimbo la Mtera ambalo ni ngome ya CCM, Lowassa aliulizwa maswali yafuayo:
"Ulipokuwa waziri mkuu ulijenga hospitali ngapi? Wewe unatuhumiwa katika Richmond na tatu wamasai wamekuwa na tabia ya kufanya vurugu na kuingiza mifugo katika mashamba ya wakulima. Sasa kama umeshindwa kuwatuliza wamasai huko kwenu, utaweza kumaliza vipi migogro ya ardhi? Aliuliza Michael Makanyi kwenye mkutano huo uliofanyika uwanja wa shule ya msingi Mvumi.
Akijibu maswali hayo, Lowassa ambaye alikuwa waziri mkuu kwa miaka miwili kutokana na sakata hilo alisema, "maswali yako mawili ya mwisho hayana maana (swali la Richmond na wamasai) ila la kwanza najibu".
Katika mkutano huo mkazi mwingine wa kijiji hicho, Daniel Makabali alimuuliza Lowassa alikisaidiaje kijiji cha Mvumi kutatua tatizo la maji na barabara alipokuwa waziri mkuu, akihoji; "Leo hii unataka kutusaidia, utawezaje wakati kipindi hicho ulishindwa?"
"Wananchi wa Mvumi mna mambo mengi sana," alisema Lowassa huku akicheka.
"Nilikuja hapa nikiwa waziri na pia nimewahi kuja kumtembelea(Waziri mkuu wa zamani)John Malecela. Nimewahi kuja mara kadhaa katika hospitali kubwa iliyopo hapa. Nimejitahidi kwa uwezo wangu wote kushughulikia matatizo ya hapa na wananchi wote wa Tanzania. Nawashukuru kwa mapokezi yenu nawashukuru kwa maswali yenu," alisema Lowassa.
Lowassa, ambaye amekuwa akitoa hotuba fupi zisizo zidi dakika 20 kwenye mikutano yake, huko Mvumi aliamua kutohutubia na badala yake aliruhusu wananchi wamuulize maswali.
Waziri huyo mkuu wa kwanza wa serikali ya awamu ya nne, amekuwa hazungumzii sakata hilo na inapotokea kulizungumzia amekuwa akieleza kuwa alijiuzulu kisiasa kuilinda serikali ya CCM na kwamba ushiriki wake ulitokana na maagizo kutoka juu.
Baada ya kutoa nafasi kwa wananchi kuuliza maswali , Michael Makanyi alitaka kufahamu kama Lowassa anahusika katika sakata hilo linalohusu kuipa Richmond Development Company ya Marekani zabuni ya kufua umeme wa dharura wakati nchi ilipokuwa na tatizo kubwa la ukosefu wa nishati hiyo mwaka 2006.
Wakati akiwa waziri mkuu 2007, Lowassa aliwahi kuruhusu swali katika mkutano uliofanyika Ukerewe, mwnafunzi aliejitambulisha kwa jina la Aron Wambura wa shule ya sekondari ya Pius Msekwa, alimuuliza wamekuwa wakiwaambia kuwa mshika mawili moja humponyoka na kuwa vijana ni taifa la kesho, hivyo wasome ili kulitumikia taifa.
"Vipi wao (viongozi) wamekuwa wakirundikiana vyeo zaidi ya kimoja kama kumteua Dk. Alex James Msekela kuwa mkoa wa Mwanza wakati pia ni mbunge?"
Swali hilo Lowassa hakulijibu.
Sasa SWALI KUU ni, "kama hawezi kujibu maswali yetu kwa hoja atawezaje kwa vitendo? Watanzania wanahitaji Kiongozi anaeweza kujibu maswali yao yote wanayo yauliza kila siku. Lowassa hawezi kabisa kuwajibu watanzania hoja zao. Jibu la hoja na maswali ya wa Tanzania ni Dk. John Pombe Magufuli.
Tafakari kwa makini na ufanye maamuzi sahihi.
Mchague kiongozi atakae leta mabadiliko yaliyo bora. Kiongozi shupavu, muadilifu na makini. Chagua CCM, chagua MAGUFULI.

EmoticonEmoticon